Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 58 · Aya ya 18

Al-Mujaadila 58:18

المجادلة

يَوْمَ يَبْعَثُهُمُ ٱللَّهُ جَمِيعًا فَيَحْلِفُونَ لَهُۥ كَمَا يَحْلِفُونَ لَكُمْ ۖ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ عَلَىٰ شَىْءٍ ۚ أَلَآ إِنَّهُمْ هُمُ ٱلْكَـٰذِبُونَ

Maana

Siku atakayowafufua Mwenyezi Mungu wote, wamuapie kama wanavyokuapieni nyinyi. Na watadhani kuwa wamepata kitu! Kwa hakika hao ndio waongo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku atakayo wafufua Mwenyezi Mungu wote, wamuwapie kama wanavyo kuwapieni nyinyi. Na watadhani kuwa wamepata kitu! Kwa hakika hao ndio waongo. [18]

[18] Siku atapo wafufua Mwenyezi Mungu wote watamwapia kuwa hakika wao walikuwa ni Waumini, kama wanavyo kuapieni nyinyi hivi sasa. Na wanadhani kuwa kwa kuapa kwao huku ni ujanja utakao wafaa. Ama kweli, hakika hawa wamefika ukomo wa uwongo!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Siku ya Kiyama, Allah Mtukufu Atawafufua wanafiki wote kutoka makaburini mwao wakiwa hai, na hapo wamuapie kuwa wao walikuwa Waumini kama walivyokuwa wakiwaapia nyinyi, (enyi Waumini), duniani. Na watadhani kuwa hilo litawanufaisha kwa Allah Mtukufu kama lilivyokuwa linawanufaisha ulimwenguni kwa Waislamu. Basi jua na utanabahi kuwa wao ndio waliofikia upeo katika urongo ambao hawakuufikia wasiokuwa wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mujaadila

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net