Al-Mujaadila 58:14
المجادلةأَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ تَوَلَّوْا۟ قَوْمًا غَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيْهِم مَّا هُم مِّنكُمْ وَلَا مِنْهُمْ وَيَحْلِفُونَ عَلَى ٱلْكَذِبِ وَهُمْ يَعْلَمُونَ
Huwaoni wale waliofanya urafiki mwendani na watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia? Hao si katika nyinyi, wala si katika wao. Na huapa kwa uongo hali ya kuwa wanajua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Huwaoni wale walio fanya urafiki na watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia? Hao si katika nyinyi, wala si katika wao. Na huapa kwa uwongo, na hali kuwa wanajua. [14]
[14] Ewe Mtume! Huwaoni wanaafiki walio wafanya marafiki watu ambao Mwenyezi Mungu ameghadhibika nao. Hawa wanao fanya urafiki si katika nyinyi, na hao wanao fanywa ni marafiki pia si katika nyinyi. Na wanaapa kwa uwongo, na huku wanajua kuwa wao ni waongo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, huwaoni wanafiki waliowafanya Mayahudi ni marafiki na wakawategemea? Na wanafiki kihakika si miongoni mwa Waislamu wala mayahudi, na wanaapa urongo kuwa wao ni Waislamu, na kuwa wewe ni Mtume wa Allah Mtukufu, na hali wanajua kuwa wao ni warongo kwa kile walichokiapia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net