Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 58 · Aya ya 13

Al-Mujaadila 58:13

المجادلة

ءَأَشْفَقْتُمْ أَن تُقَدِّمُوا۟ بَيْنَ يَدَىْ نَجْوَىٰكُمْ صَدَقَـٰتٍ ۚ فَإِذْ لَمْ تَفْعَلُوا۟ وَتَابَ ٱللَّهُ عَلَيْكُمْ فَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ ۚ وَٱللَّهُ خَبِيرٌۢ بِمَا تَعْمَلُونَ

Maana

Mnachelea kutanguliza hiyo sadaka kabla ya kusemezana kwenu kwa siri? Ikiwa hamkufanya hayo, na Mwenyezi Mungu akapokea toba yenu, basi simamisheni Sala, na toeni Zaka, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mnachelea kutanguliza hiyo sadaka kabla ya kusemezana kwenu? Ikiwa hamkufanya hayo, na Mwenyezi Mungu akapokea toba yenu, basi shikeni Swala, na toeni Zaka, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. [13]

[13] Mnachelea kujilazimisha kutoa sadaka kabla ya mazungumzo yenu na Mtume wa Mwenyezi Mungu? Na ikiwa hamkutoa, na Mwenyezi Mungu akakusameheni, basi hifadhini kushika Swala na kutoa Zaka, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za vitendo vyenu, naye atakulipeni kwavyo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, mmeogopa kuwa mtapata umaskini mkitanguliza sadaka kabla ya kunong’ona na Mtume wa Allah Mtukufu? Basi msipofanya hilo mliloamrishwa, (na Allah Mtukufu Amewasamehe na Amewaruhusu msilifanye hilo), basi simameni imara na muendelee kusimamisha Swala, kutoa Zaka na kumtii Allah Mtukufu na Mtume Wake katika kila lile mliloamrishwa. Na Allah Mtukufu ni Mtambuzi wa Matendo yenu, na ni Mwenye kuwalipa kwayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mujaadila

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net