Al-Waaqia 56:70
الواقعةلَوْ نَشَآءُ جَعَلْنَـٰهُ أُجَاجًا فَلَوْلَا تَشْكُرُونَ
Tungelipenda, tungeliyafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru? [70]
[70] Lau tungeli taka tungeli yafanya hayo maji yakawa ya chumvi yasiyo nyweka. Basi mbona hamumshukuru Mwenyezi Mungu aliye yajaalia matamu yenye kunyweka?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Lau tungetaka tungeyafanya maji haya yawe na chumvi sana, ikawa haiwezekani kunufaika nayo kwa kunywa wala kwa mimea. Basi si mumshukuru Mola wenu kwa kuteremsha maji tamu kwa kuwanufaisha nyinyi?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net