Al-Waaqia 56:69
الواقعةءَأَنتُمْ أَنزَلْتُمُوهُ مِنَ ٱلْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ ٱلْمُنزِلُونَ
Je, ni nyinyi mnaoyateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha? [69]
[69] Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni, au ni Sisi ndio Wenye kuyateremsha kuwa ni rehema juu yenu? Katika Kiarabu limetajwa neno Almuzni. Maana yake ni mawingu yanayo leta mvua. Na kitendo cha kunyesha mvua kinahitajia mambo yaliyo khusiana na hali ya hewa maalumu ambayo mwanaadamu hana mamlaka nayo, au kuyaleta kwa juhudi zake. Kwa mfano zinahitajiwa pepo zinazo kwenda kwa mkondo zilizo baridi juu ya nyengine zilizo za joto, au hali za kuondoka utulivu katika anga. Na watu wamejaribu kuinyesha mvua kwa mawingu yanayo pita kwa njia ya ufundi, lakini juhudi hizo mpaka sasa ni majaribio, na lilio thibiti katika sayansi ni kufuzu kwa majaribio hayo ni kudogo mno, na hata hivyo kunalazimu ziwepo hali maalumu za maumbile zinazo saidia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je ni nyinyi mliyoyateremsha kutoka kwenye mawingu hadi kwenye kituo cha ardhi au ni sisi tuliyoyateremsha ili kuwarehemu nyinyi?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net