Al-Qamar 54:51
القمروَلَقَدْ أَهْلَكْنَآ أَشْيَاعَكُمْ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anayekumbuka?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka? [51]
[51] Na bila ya shaka Sisi tumekwisha waangamiza wengine walio fanana nanyi katika ukafiri. Je! Yupo aliye waidihika?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika tuliwaangamiza wale waliofanana na nyinyi katika ukafiri miongoni mwa ummah waliopita. Basi je, kuna mwenye kuwaidhika kwa mateso na adhabu?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net