Al-Qamar 54:50
القمروَمَآ أَمْرُنَآ إِلَّا وَٰحِدَةٌ كَلَمْحٍۭ بِٱلْبَصَرِ
Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho. [50]
[50] Na haikuwa amri yetu tukitaka kitu ila neno moja tu, nalo ni kusema: "Kuwa", nacho huwa, papo hapo kama kupepesa kwa jicho.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tukitaka jambo liwe tunasema neno moja tu, nalo ni «kuwa» nalo linakuwa hapohapo kama vile kupepesa jicho.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net