Al-Qamar 54:44
القمرأَمْ يَقُولُونَ نَحْنُ جَمِيعٌ مُّنتَصِرٌ
Au ndiyo wanasema: 'Sisi ni wengi tutashinda tu.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu. [44]
[44] Bali ati wanasema hawa makafiri: Sisi ni kikundi kilicho ungana chenye nguvu juu ya maadui wake, hakishindwi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au kwani wanasema makafiri wa Makkah, «Sisi ndio wenye ushupavu na busara, na jambo letu ni la pamoja. Sisi ni watu wa ushindi, na hatatushinda anayetutaka kwa ubaya.?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net