Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 54 · Aya ya 43

Al-Qamar 54:43

القمر

أَكُفَّارُكُمْ خَيْرٌ مِّنْ أُو۟لَـٰٓئِكُمْ أَمْ لَكُم بَرَآءَةٌ فِى ٱلزُّبُرِ

Maana

Je, makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani? [43]

[43] Ati nyinyi, makafiri, mna nguvu zaidi kuliko hao wa kaumu zilizo tangulia ambao wameangamizwa? Au nyinyi mmetolewa makosani kwa ilivyo teremka katika Vitabu vya mbinguni?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je makafiri wenu, (enyi mkusanyiko wa makureishi), ni bora kuliko wale waliotangulia kutajwa miongoni mwa wale walioangamia kwa sababu ya kukanusha kwao? Au nyinyi mmeepushwa na mateso ya Allah Mtukufu kwa yaliyomo kwenye Vitabu vilivyoteremshwa kwa Mitume kuwa mtasalimika na mateso?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qamar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net