Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 54 · Aya ya 15

Al-Qamar 54:15

القمر

وَلَقَد تَّرَكْنَـٰهَآ ءَايَةً فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ

Maana

Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anayekumbuka?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye kumbuka? [15]

[15] Na tumeliacha hilo tukio na kuzamishwa makafiri na kuokolewa Waumini liwe ni mawaidha, lakini yupo mwenye kuwaidhika?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa hakika tulikibakisha kisa cha Nûḥ pamoja na watu wake kiwe ni mazingatio na dalili ya uwezo wetu kwa walio baada ya Nûḥ, ili wazingatie na wawaidhike kwa lililowapata ummah huu uliokanusha Mtume wao, je kuna wa kuwaidhika awaidhike?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qamar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net