Al-Qamar 54:14
القمرتَجْرِى بِأَعْيُنِنَا جَزَآءً لِّمَن كَانَ كُفِرَ
Ikawa inakwenda kwa macho yetu, kuwa ni malipo kwa aliyekuwa amekanushwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa. [14]
[14] Likawa linakwenda baharini chini ya hifadhi yetu, kuwa ni malipo kwa Nuhu ambaye watu wake waliendelea kuukanya wito wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ikawa inatembea kwa uangalizi wetu na utunzi, na tukawazamisha waliokanusha, ikiwa ni malipo yao kwa ukafiri wao na kwa kumnusuru Nûḥ, (amani imshukie). Hapa pana dalili ya kuthibitisha sifa ya macho mawili kwa Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, kama inavyonasibiana naye.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net