An-Najm 53:43
النجموَأَنَّهُۥ هُوَ أَضْحَكَ وَأَبْكَىٰ
Na kwamba Yeye ndiye anayeleta kicheko na kilio.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio. [43]
[43] Na Yeye peke yake ni Mwenye uweza wa kuufanya uso uonyeshe furaha au maudhiko, na pia ni Mwenye kuziumba sababu za starehe na dhiki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwamba Yeye, (Aliyetukuka na kutakasika), Ndiye Anayemfanya Anayemtaka acheke duniani kwa kumfurahisha, na ndiye Anayemfanya Anayemtaka aliye kwa kumpa mitihani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net