An-Najm 53:27
النجمإِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ تَسْمِيَةَ ٱلْأُنثَىٰ
Hakika wale wasioamini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike. [27]
[27] Hakika hao wasio iamini Akhera ndio bila ya shaka wanao sema kuwa Malaika ni wanawake. Wanasema: Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale ambao hawaamini kuwa kuna maisha ya Akhera miongoni mwa makafiri wa Kiarabu, wala hawafanyi matendo ya kuwafaa huko, wanawaita Malaika majina ya kike, kwa kuitakidi kwao kuwa Malaika ni wanawake, na kuwa wao ni watoto wa kike wa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net