At-Tur 52:41
الطورأَمْ عِندَهُمُ ٱلْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ
Au wanayo elimu ya ghaibu, nao wameandika?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wameandika? [41]
[41] Bali kwani wao wanao ujuzi kujua mambo ya ghaibu, yaliyo fichikana, na hivyo wanaandika kutoka hayo wayatakayo?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au wao wana ujuzi wa ghaibu wakawa wanawaandikia watu na kuwapa habari yake? Mambo si hivyo, kwani hakika ya mambo ni kwamba hakuna anayejua ghaibu iliyo mbinguni na ardhini isipokuwa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net