At-Tur 52:40
الطورأَمْ تَسْـَٔلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ
Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama? [40]
[40] Kwani wewe unawaomba chochote kuwa ni ujira wa kuwafikishia Ujumbe wako, ndio wamethakilika na hizo gharama wakalalimika?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au unawataka, (ewe Mtume), hawa washirikina wakupatie malipo ya kuwafikishia Ujumbe? wakawa wanaona tabu na dhiki ya kujilazimisha malipo unayoyataka kutoka kwao?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net