At-Tur 52:38
الطورأَمْ لَهُمْ سُلَّمٌ يَسْتَمِعُونَ فِيهِ ۖ فَلْيَأْتِ مُسْتَمِعُهُم بِسُلْطَـٰنٍ مُّبِينٍ
Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja iliyo wazi!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja ilio wazi! [38]
[38] Bali wanacho kipandio cha kupandia mpaka mbinguni wakasikiliza anayo yahukumia Mwenyezi Mungu? Kama hivyo, basi nawamlete huyo mtu wao anaye sikiliza atoe hoja iliyo wazi kuthibitisha madai yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au wao wana ngazi ya kupandia mbinguni wanasikiliza huko wahyi kwamba yale waliyonayo ndio haki? Basi na aje, yule anayedai kuwa amesikia hilo, na hoja ya waziwazi yenye kusadikisha madai yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net