At-Tur 52:37
الطورأَمْ عِندَهُمْ خَزَآئِنُ رَبِّكَ أَمْ هُمُ ٱلْمُصَۣيْطِرُونَ
Au wanazo hazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka? [37]
[37] Kwani wao wanazo khazina za Mola wako Mlezi wanazo zisarifu watakavyo? Au wana nguvu za kutenda watakavyo, na kupanga mambo kama wapendavyo?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au wanazo wao hazina za Mola wako wanazitumia? Au wao ni majabari wanaowagandamiza viumbe vya Allah Mtukufu kwa kuwatendesha nguvu na kuwanyanyasa? Mambo si hivyo, bali wao ndio walioelemewa na waliyo madhaifu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net