Adh-Dhaariyat 51:29
الذارياتفَأَقْبَلَتِ ٱمْرَأَتُهُۥ فِى صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌ
Ndipo mkewe akawaelekea kwa sauti ya kelele huku anajipiga usoni kwa mastaajabu, akasema: "Mimi ni kikongwe na tasa!"
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa! [29]
[29] Akatokea mkewe akipiga kelele alipo isikia ile bishara, akijipiga uso wake kwa mkono wake, kwa kuona muhali hayo na kustaajabu, na akasema: Mimi ni kizee, na tasa. Itakuwaje nizae?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Aliposikia mke wa Ibrãhîm maneno ya bishara ya hao Malaika, alielekea upande wao akiwa anapiga ukelele, akajipiga uso wake kwa kulionea ajabu jambo hili na akasema, «Vipi nitazaa na mimi ni tasa sizai?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net