Adh-Dhaariyat 51:28
الذارياتفَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۖ قَالُوا۟ لَا تَخَفْ ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَـٰمٍ عَلِيمٍ
Kwa hivyo, akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: 'Usiwe na hofu.' Basi wakambashiria kupata kijana mwenye elimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu. [28]
[28] Akahisi katika nafsi yake khofu kuwaogopa. Wakasema: Usiogope. Na wakampa bishara kuwa atapata mwana mwenye ilimu nzuri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Alipowaona hawali aliingiwa na hofu ya kuwaogopa, na hapo wakamuambia, «Usiogope! Sisi ni wajumbe wa Allah Mtukufu. Na wakampa bishara kwamba mkewe Sārah atamzalia mtoto atakayekuwa miongoni mwa watu wanaomjua Allah Mtukufu na kuijua Dini Yake, (naye ni Isḥāq), amani imshukie».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net