Qaaf 50:17
قإِذْ يَتَلَقَّى ٱلْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ ٱلْيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ قَعِيدٌ
Wanapopokea wapokeaji wawili, wanaokaa kuliani na kushotoni.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanapo pokea wapokeaji wawili, wanao kaa kuliani na kushotoni. [17]
[17] Watakapo kutana Malaika wawili walinzi, mmoja anakaa kuliani, na mwingine anakaa upande wa kushoto, wakiviandika vitendo vyake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Pindi Malaika wawili wanaotunza, kuliani kwake na kushotoni kwake, wanapoyaandika matendo Yake: aliye kuliani anaandika mema na aliye kushotoni anaandika maovu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net