Qaaf 50:16
قوَلَقَدْ خَلَقْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِۦ نَفْسُهُۥ ۖ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ ٱلْوَرِيدِ
Na hakika tulimuumba mtu, nasi tunayajua yanayomtia wasiwasi katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitikia katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake. [16]
[16] Ninaapa: Bila ya shaka tumemuumba mtu, na Sisi tunajua hata anayo semezwa na nafsi yake. Na Sisi kwa kuzijua hali zake zote, ni karibu kuliko mshipa wake wa damu ulioko shingoni mwake. Na hicho ndicho kitu kilicho karibu mno naye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hakika tumemuumba binadamu na tunakijua kile ambacho nafsi yake inamhadithia kwacho. Na sisi tuko karibu naye zaidi kuliko ukamba wa roho (nao ni mshipa ulioko shingoni unaoshikana na moyo).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net