Al-Hujuraat 49:1
الحجراتيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تُقَدِّمُوا۟ بَيْنَ يَدَىِ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Enyi mlioamini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia mno, Mwenye kujua zaidi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. [1]
[1] Enyi mlio amini! Msitangulie na kulikata jambo lolote la kidini na la kidunia bila ya kukuamrisheni Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na jiwekeeni kinga ya nafsi zenu isikupateni adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata sharia yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia baraabara yote mnayo yasema, ni Mwenye kuyajua vilivyo mambo yote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake msiamue jambo la Sheria za Dini yenu kinyume cha maamuzi ya Allah Mtukufu na Mtume Wake, mkaingia kwenye uzushi. Na muogopeni Allah Mtukufu katika maneno yenu na vitendo vyenu, isije amri ya Allah Mtukufu na Mtume Wake ikaendewa kinyume. Hakika Allah Mtukufu ni Msikizi wa maneno yenu, ni Mjuzi wa nia zenu na vitendo vyenu. Hapa pana onyo kwa Waumini wasifanye uzushi katika Dini au kuleta sheria ambazo Allah Mtukufu Hakuziruhusu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net