Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 48 · Aya ya 21

Al-Fath 48:21

الفتح

وَأُخْرَىٰ لَمْ تَقْدِرُوا۟ عَلَيْهَا قَدْ أَحَاطَ ٱللَّهُ بِهَا ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرًا

Maana

Na yale mengine hamwezi kuyapata bado, Mwenyezi Mungu amekwisha yazingira. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza mno wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mengine hamwezi kuyapata bado, Mwenyezi Mungu amekwisha yazingia. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hakika Allah Mtukufu Amewaahidi nyinyi ngawira nyingine ambayo hamna uwezo nayo, Allah Mtukufu, kutakasika na kutukuka ni Kwake, Ndiye Mwenye uwezo nayo, nayo iko chini ya mpango Wake na mamlaka Yake, na Ashawaahidi nyinyi kuwapatia, na hapana budi kwamba kile Alichoahidi kitakuwa. Na Allah Mtukufu juu ya kila kitu ni Muweza, hakuna chochote kinachomshinda.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Fath

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net