Al-Fath 48:20
الفتحوَعَدَكُمُ ٱللَّهُ مَغَانِمَ كَثِيرَةً تَأْخُذُونَهَا فَعَجَّلَ لَكُمْ هَـٰذِهِۦ وَكَفَّ أَيْدِىَ ٱلنَّاسِ عَنكُمْ وَلِتَكُونَ ءَايَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ وَيَهْدِيَكُمْ صِرَٰطًا مُّسْتَقِيمًا
Mwenyezi Mungu anawaahidi ngawira nyingi mtakazozichukua, basi amewatangulizia hizi kwanza, na akaizuia mikono ya watu isiwafikie, na ili hayo yawe ni Ishara kwa Waumini, na akawaongoza njia iliyonyooka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu anakuahidini ngawira nyingi mtakazo zichukua, basi amekutangulizieni hizi kwanza, na akaizuia mikono ya watu isikufikieni, na ili hayo yawe ni Ishara kwa Waumini, na akakuongozeni Njia Iliyo Nyooka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Amewaahidi nyinyi ngawira nyingi mtakazozichukua katika nyakati zake alizowakadiria, Akawaharakishia ngawira za (Khaybar) na Akaizuia mikono ya watu isiwafikie nyinyi, lisiwapate ovu lolote kati ya yale maovu ambayo maadui wenu waliyadhamiria ya vita na mapigano, na lisiwapate wale mliowaacha Madina, na ili kule kushindwa kwao, kusalimika kwenu na kupata ghanima kwenu kuwe ni alama ya nyinyi kuizingatia na kuchukua dalili kwayo kuwa Allah Mtukufu Ndiye Mwenye kuwahifadhi nyinyi na kuwanusuru, na yeye Ndiye Anayewaongoza kwenye njia iliyonyooka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net