Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 47 · Aya ya 21

Muhammad 47:21

محمد

طَاعَةٌ وَقَوْلٌ مَّعْرُوفٌ ۚ فَإِذَا عَزَمَ ٱلْأَمْرُ فَلَوْ صَدَقُوا۟ ٱللَّهَ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ

Maana

Utiifu na kauli njema. Na jambo likishaazimiwa, basi wakiwa ni wakweli kwa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka itakuwa ni heri kwao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ut'iifu na kauli njema. Na jambo likisha azimiwa, basi wakiwa ni wakweli kwa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka itakuwa ni kheri kwao. [21]

[21] Na mambo yakawa ni kweli, na ikawalazimu kupigana, basi lau kuwa ni kweli wana Imani ya Mwenyezi Mungu na ut'iifu ingeli kuwa bora kwao kuliko huo unaafiki. Basi ndio mnavyo tarajiwa, enyi wanaafiki, kuwa mkipata madaraka ndio mfisidi katika nchi na mkate makhusiano yenu na jamaa zenu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi lililo bora kwa hawa ambao ndani ya nyoyo zao mna maradhi wamtii Allah Mtukufu na waseme neno linaloafikiana na Sheria. Vita vinapopasa na ikaja amri ya Allah Mtukufu kuilazimisha, hawa wanafiki wanachukia hilo. Na lau wao wangekuwa wakweli kwa Allah Mtukufu katika kuamini na kutenda mema, hilo lingekuwa bora kwao kuliko kufanya maasia na kuenda kinyume.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Muhammad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net