Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 47 · Aya ya 20

Muhammad 47:20

محمد

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَوْلَا نُزِّلَتْ سُورَةٌ ۖ فَإِذَآ أُنزِلَتْ سُورَةٌ مُّحْكَمَةٌ وَذُكِرَ فِيهَا ٱلْقِتَالُ ۙ رَأَيْتَ ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ نَظَرَ ٱلْمَغْشِىِّ عَلَيْهِ مِنَ ٱلْمَوْتِ ۖ فَأَوْلَىٰ لَهُمْ

Maana

Na Waumini wanasema: 'Kwa nini haiteremshwi Sura?' Na inapoteremshwa Sura madhubuti na ikatajwa ndani yake habari ya vita, utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anayezimia kwa sababu ya mauti. Basi ni bora kwao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Waumini wanasema: Kwa nini haiteremshwi Sura? Na inapo teremshwa Sura madhubuti na ikatajwa ndani yake khabari ya vita, utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anaye zimia kwa mauti. Basi ni bora kwao [20]

[20] Walio amini wanasema: Haiteremki Sura ya kututaka tupigane? Na ikiteremka Sura ambayo haifasiriki vyenginevyo ila ni kulazimisha tu, na ikataja ndani yake kuamrishwa vita, utawaona ambao katika nyoyo zao mna unaafiki wanakuangalia kwa muangalio wa mwenye kuzimia kwa mauti, jinsi ya kuviogopa na kuvichukia vita. Linalo wastahikia kulifanya ni kumt'ii Mwenyezi Mungu na kusema neno linalo kubaliana na sharia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale wanaomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake wanasema, «Basi si iteremshwe sura kutoka kwa Allah Mtukufu ituamrishe kupigana jihadi na wakanushaji.» Na inapoteremshwa sura iliyoimarika kwa maelezo na mambo ya lazima na ikatajwa jihadi ndani yake, utawaona wale ambao mna shaka ndani ya nyoyo zao juu ya Dini ya Allah Mtukufu na unafiki wanakuangalia, ewe Nabii, maangalizi ya mtu ambaye amefunikwa na hofu ya kufa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Muhammad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net