Muhammad 47:18
محمدفَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا ٱلسَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً ۖ فَقَدْ جَآءَ أَشْرَاطُهَا ۚ فَأَنَّىٰ لَهُمْ إِذَا جَآءَتْهُمْ ذِكْرَىٰهُمْ
Kwani wanangojea jengine isipokuwa iwafikie Saa (ya Kiyama) kwa ghafla? Na hakika alama zake zimekwisha kuja. Na itakapowajia, kutawafaa nini kukumbuka kwao?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwani wanangojea jengine isipo kuwa iwafikie Saa (ya Kiyama) kwa ghafla? Na hakika alama zake zimekwisha kuja. Na itapo wajia kutawafaa wapi kukumbuka hapo? [18]
[18] Wanao kanusha hawawaidhiki na hali za walio tangulia. Basi je! Wanangojea Saa (ya Kiyama) iwajie kwa ghafla? Kwa hakika alama zake zimekwisha dhihiri, na wao hawajazingatia kuwa inakuja. Basi watakumbuka wapi itapo wajia mara moja kwa ghafla?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakanushaji hawa hawangojei isipokuwa wakati wa Kiyama ambao wameahidiwa kuwa utawajia kwa ghafla. Kwani alama zake zishajitokeza na wao hawakunufaika nazo. Basi watapata wapi kukumbuka wakati wa Kiyama utakapowajia?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net