Muhammad 47:17
محمدوَٱلَّذِينَ ٱهْتَدَوْا۟ زَادَهُمْ هُدًى وَءَاتَىٰهُمْ تَقْوَىٰهُمْ
Na wale walioongoka anawazidishia uongofu na anawapa ucha Mungu wao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale walio ongoka anawazidishia uongofu na anawapa uchamngu wao. [17]
[17] Na walio ongoka wakashika njia ya Haki, Mwenyezi Mungu huwazidishia uwongofu, na akawapa kinga chao cha kujikingia na Moto.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale walioongoka kuifuata haki, Allah Mtukufu Aliwaongezea uongofu, na kwa hivyo uongofu wao ukapata nguvu na Akawaafikia kwenye uchamungu na akaufanya sahali kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net