Muhammad 47:14
محمدأَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِۦ كَمَن زُيِّنَ لَهُۥ سُوٓءُ عَمَلِهِۦ وَٱتَّبَعُوٓا۟ أَهْوَآءَهُم
Je, yule aliye kwenye ubainifu kutoka kwa Mola wake Mlezi ni kama yule aliyepambiwa uovu wa vitendo vyake, na wakafuata matamanio yao?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Mwenye kuwa na bayana kutoka kwa Mola wake Mlezi ni kama aliye pambiwa uovu wa vitendo vyake, na wakafuata pumbao lao? [14]
[14] Je! Wanaweza kuwa sawa makundi mawili haya katika malipo? Mwenye kuwa na ujuzi wazi kumjua Muumba wake na Mlezi wake, naye akawa anamt'ii, atakuwa sawa na mwenye kuwa na vitendo vyake viovu naye akaviona ni vizuri, na akafuata hayo ayatendayo na akaeneza pumbao lake la upotovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je yule aliyekuwa na ushahidi ulio wazi kutoka kwa Allah Mtukufu na ujuzi kuwa Yeye ni Mmoja, analingana na yule ambaye Shetani amempambia matendo yake maovu na akafuata yale ambayo nafsi yake ilimuita iyafuate ya kumuasi Allah Mtukufu na kumuabudu asiyekuwa Yeye bila ya hoja wala ushahidi? Hawalingani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net