Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 47 · Aya ya 13

Muhammad 47:13

محمد

وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ هِىَ أَشَدُّ قُوَّةً مِّن قَرْيَتِكَ ٱلَّتِىٓ أَخْرَجَتْكَ أَهْلَكْنَـٰهُمْ فَلَا نَاصِرَ لَهُمْ

Maana

Na ni miji mingapi iliyokuwa na nguvu zaidi kuliko mji wako huu uliokutoa? Tuliwateketeza na wala hawakuwa na yeyote wa kuwanusuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na miji mingapi iliyo kuwa na nguvu zaidi kuliko mji wako huu ulio kutoa; nao tuliwateketeza na wala hawakuwa wa kuwanusuru. [13]

[13] Na wengi katika watu wa miji walio tangulia walio kuwa na nguvu zaidi kushinda watu wa mji wako wa Makka ambao watu wake wamekufukuza, ewe Muhammad, tuliwaangamiza kwa namna mbali mbali za adhabu. Na hakutokea yeyote wa kuwanusuru nasi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wengi miongoni mwa watu wa mijini walikuwa wana nguvu zaidi kuliko watu wa mji wako, ewe Mtume, ambao ni Makkah, (waliokutoa watu wake humo). Watu wa miji hiyo tuliwaangamiza kwa adhabu za aina mbalimbali. Hawakuwa na msaidizi wa kuwanusuru kutokana na adhabu ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Muhammad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net