Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 47 · Aya ya 11

Muhammad 47:11

محمد

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ مَوْلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَأَنَّ ٱلْكَـٰفِرِينَ لَا مَوْلَىٰ لَهُمْ

Maana

Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa wale walioamini. Na makafiri hawana mlinzi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Na makafiri hawana mlinzi. [11]

[11] Malipo hayo ndio ushindi wa Waumini na kushindwa nguvu makafiri, ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ni rafiki mlinzi wa walio amini na ndiye Mwenye kuwanusuru; na makafiri hawana rafiki mlinzi wa kuwanusuru wala kuwakinga na kuangamia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hilo tulilowafanyia watu wa mapote mawili: pote la Imani na pote la ukafiri, ni kwa kuwa Allah Mtukufu Ndiye Msimamizi wa Waumini na mwenye kuwanusuru, na kuwa makafiri hawana mwenye kuwasimamia wala kuwanusuru.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Muhammad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net