Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 47 · Aya ya 10

Muhammad 47:10

محمد

أَفَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ دَمَّرَ ٱللَّهُ عَلَيْهِمْ ۖ وَلِلْكَـٰفِرِينَ أَمْثَـٰلُهَا

Maana

Kwani hawakutembea katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Mwenyezi Mungu aliwaangamiza, na kwa makafiri hawa itakuwa mifano ya hayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwani hawakutembea katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa walio kuwa kabla yao? Mwenyezi Mungu aliwaangamiza, na kwa makafiri hawa itakuwa mfano wa hayo. [10]

[10] Wameshindwa kutafuta ya kuwazindua, hata hawakutembea katika ardhi wakaangalia hali gani ulikuwa mwisho wa walio wakadhibisha Mitume kabla yao? Mwenyezi Mungu aliwateremshia hilaki katika kila kilicho khusiana nao, nafsi zao, mali yao, na watoto wao. Na wenye kumkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake ndio hupata mwisho mfano wa huo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hawakwenda makafiri hawa kwenye ardhi ya Allah Mtukufu wakayazingatia yale yaliyowapata ummah waliopita ya mateso? Allah Mtukufu Aliyavunjavunja majumba yao. Na makafiri hawa watakuwa na mwisho kama huo uliowafikia ummah hao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Muhammad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net