Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 45 · Aya ya 23

Al-Jaathiya 45:23

الجاثية

أَفَرَءَيْتَ مَنِ ٱتَّخَذَ إِلَـٰهَهُۥ هَوَىٰهُ وَأَضَلَّهُ ٱللَّهُ عَلَىٰ عِلْمٍ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمْعِهِۦ وَقَلْبِهِۦ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِۦ غِشَـٰوَةً فَمَن يَهْدِيهِ مِنۢ بَعْدِ ٱللَّهِ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Maana

Je, umemwona aliyefanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akampoteza pamoja na kuwa ana elimu, na akaziba masikio yake, na moyo wake, na akambandika kifuniko kwenye kuona kwake? Basi ni nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Je, hamkumbuki?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki? [23]

[23] Ewe Mtume! Umeangalia, ukamwona huyo mwenye kufanya matamanio yake ndiye mungu wake wa kumuabudu, akamnyenyekea, na akamt'ii, na akaiacha Njia ya Haki na hali anaijua, na akaziba masikio yake asisikie waadhi, na moyo wake asiamini Haki, na akabandika vitanga vya macho asione ya kuzingatiwa? Basi nani wa kumwongoa mtu huyu baada ya kwisha puuzwa na Mwenyezi Mungu? Je! Mnaacha kutazama ili msipate kukumbuka?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Unamuonaje ewe Mtume, yule aliyeyachukua matamanio yake akayafanya ndiye Mola wake, akawa hatamani kitu isipokuwa anakifanya kwa matamanio yake, na Allah Mtukufu Akampoteza baada ya ujuzi kumfikia na kusimamiwa na hoja, akawa hasikii mawaidha ya Allah Mtukufu wala hazingatii kwa mawaidha hayo, na Allah Mtukufu akapiga mhuri kwenye moyo wake akawa hafahamu kitu, na Akaweka funiko kwenye macho yake akawa hazioni hoja za Allah Mtukufu? Basi ni nani atakayemuongoza kuifikia haki na uongofu baada ya Allah Mtukufu kumpoteza? Kwani hamkumbuki, enyi watu, mkajua kwamba mwenye kufanywa hivyo na Allah Mtukufu hataongoka kabisa na hatapata wa kumsaidia na kumuongoza? Aya hii ndio msingi wa kuonya kuwa matamanio hayafai kuwa ndio msukumo wa Waumini katika matendo yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jaathiya

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net