Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 45 · Aya ya 1

Al-Jaathiya 45:1

الجاثية

حمٓ

Maana

Ha Mim.[1]

[1] Herufi hizi "Ha, Mim" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

H'a Mim . [1]

[1] H'a Mim. Hizi ni harufi mbili katika harufi za kutamkwa, zimeanzia Sura hii kama ada ya Sura nyingi katika Qur'ani ambazo zimeanzia kwa harufi kama hivi ili kuashiria kuwa washirikina wameshindwa kuleta mfano wake, ijapo kuwa hii Qur'ani imeundwa kwa harufi hizi hizi wanazo zitumia katika maneno yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hā, mīm Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa katika mwanzo wa sura ya Al-Baqarah.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jaathiya

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net