Ad-Dukhaan 44:59
الدخانفَٱرْتَقِبْ إِنَّهُم مُّرْتَقِبُونَ
Ngoja tu, na wao wangoje pia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ngoja tu, na wao wangoje pia. [59]
[59] Basi wewe yangojee hayo yatakayo wafika, na wao pia wanangojea yatakayo kufika wewe na huo wito wako, mambo yakibadilika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi ngojea, ewe Mtume, ushindi niliokuahidi juu ya hawa wenye kumshirikisha Allah Mtukufu na adhabu itakayowashukia. Wao ni wenye kungojea kufa kwako, kukushinda. Basi watajua utakuwa ni wa nani ushindi, kufaulu na sauti ya juu duniani na Akhera. Hivyo ni vyako wewe, na vya wale Waumini waliokufuata.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net