Ad-Dukhaan 44:54
الدخانكَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَـٰهُم بِحُورٍ عِينٍ
Hivi ndivyo itakavyokuwa, na tutawaoza mahurilaini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini. [54]
[54] Na pamoja na malipo haya tutawaoza huko Peponi mahurulaini, ambao huwezi kuwachanganyia jicho kwa hadi ya uzuri wao na ukubwa wa macho yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kama tutakavyowapa huko Akhera takrima ya kuwaingiza Peponi na kuwavisha hariri nzito na hariri yenye mng’aro, vilevile tutawakirimu kwa kuwaozesha wanawake wazuri wenye macho makubwa ya kupendeza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net