Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 44 · Aya ya 53

Ad-Dukhaan 44:53

الدخان

يَلْبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَقَـٰبِلِينَ

Maana

Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakielekeana.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana, [53]

[53] Wakivaa humo hariri nyepesi na nzito kuzidi kuongeza mapambo yao, nao wakielekeana katika majlisi zao, ili kutimiza starehe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watakuwa wamevaa dibaji nyororo na pia nzito, hali ya kuwa wameelekeana kwa nyuso. Na hawatakuwa wakiangaliana visogo. Viti vyao watakuwa wakizunguka navyo pale wanapozunguka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ad-Dukhaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net