Ad-Dukhaan 44:42
الدخانإِلَّا مَن رَّحِمَ ٱللَّهُ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Isipokuwa yule mbaye Mwenyezi Mungu atamrehemu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. [42]
[42] Lakini wale ambao Mwenyezi Mungu amewarehemu, miongoni mwa Waumini, Mwenyezi Mungu atawasamehe, na atawapa ruhusa ya uombezi waweze kuwaombea wenginewe. Hakika Yeye ndiye Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye kuwarehemu waja wake Waumini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Isipokuwa yule ambaye Allah Mtukufu Amemrehemu miongoni mwa Waumini, kwani yeye huenda akamuombea kwa Mola wake baada ya kuruhusiwa na Allah Mtukufu. Kwa hakika Allah Mtukufu Ndiye Mshindi katika kuwatesa maadui zake, Ndiye Mwenye kuwarehemu kwa wingi wale wenye kumtegemea na kumtii.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net