Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 44 · Aya ya 41

Ad-Dukhaan 44:41

الدخان

يَوْمَ لَا يُغْنِى مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْـًٔا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ

Maana

Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa. [41]

[41] Siku ambayo jamaa hawezi kumtetea jamaa yake, wala rafiki kumtetea rafiki yake kwa lolote, hata kwa uchache wa adhabu. Wala wao hawatanusuriwa nafsi zao mbele ya Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Siku ambayo hakuna rafiki atakayeweza kumuondolea rafiki yake shida yoyote, wala hawatasaidiana wao kwa wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ad-Dukhaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net