Ad-Dukhaan 44:29
الدخانفَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ ٱلسَّمَآءُ وَٱلْأَرْضُ وَمَا كَانُوا۟ مُنظَرِينَ
Basi mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula. [29]
[29] Basi la mbingu wala ardhi hazikuwahuzunukia ilipo wanyakua adhabu, jinsi ilivyo haribika hali yao; wala hawakungojewa watubu, wala hawakupewa muhula wapate kudiriki taksiri yao, kwa jinsi walivyo dharauliwa!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mbingu na ardhi hazikulia kwa kumsikitikia Fir’awn na watu wake, na hawakuwa ni wenye kucheleshewa adhabu iliyowashukia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net