Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 44 · Aya ya 28

Ad-Dukhaan 44:28

الدخان

كَذَٰلِكَ ۖ وَأَوْرَثْنَـٰهَا قَوْمًا ءَاخَرِينَ

Maana

Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wengineo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe. [28]

[28] Mfano wa adhabu hiyo Mwenyezi Mungu humuadhibu mwenye kwenda kinyume na amri yake, na akatoka katika ut'iifu wake, na humwondolea neema yule mwenye nayo akawapa watu wenginewe wasio kuwa na makhusiano nao yoyote, la ya ujamaa wala dini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mfano wa mateso hayo ndivyo Allah Mtukufu Anavyowatesa wenye kukanusham na kubadilisha neema za Allah Mtukufu kwa kuzikanusha. Na tuliwarithisha neema hizo, baada ya Fir’awn na watu wake, watu wengine waliokuja baada yao, wakashika nafasi yao miongoni mwa Wana wa Isrãîl.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ad-Dukhaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net