Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 44 · Aya ya 17

Ad-Dukhaan 44:17

الدخان

وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَآءَهُمْ رَسُولٌ كَرِيمٌ

Maana

Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu. [17]

[17] Na bila ya shaka tulikwisha wafanyia mtihani, kabla ya makafiri wa Makka, kaumu ya Firauni kwa kuwaitia kwenye Imani, na akawajia Musa, Mtume Mtukufu kwa Mwenyezi Mungu. Wakamkataa kwa inda tu. Na huo ndio mtindo wa hawa washirikina.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika tushawafanyia mtihani na kuwajaribu watu wa Fir’awn kabla ya hawa washirikina, na aliwajia Mtume mtukufu, naye ni Mûsã, amani imshukie, wakamkanusha na wakaangamia. Basi hivi ndivyo tutakavyowafanya maadui zako, ewe Mtume, wasipoamini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ad-Dukhaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net