Ad-Dukhaan 44:16
الدخانيَوْمَ نَبْطِشُ ٱلْبَطْشَةَ ٱلْكُبْرَىٰٓ إِنَّا مُنتَقِمُونَ
Siku tutakayoyashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa. [16]
[16] Ewe Mtume! Watajie ile siku tutapo washika kwa mshiko mkubwa, wa nguvu. Nasi kwa mshiko huu ndio tunawatesa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Siku tutakayowaadhibu makafiri wote adhabu kubwa kabisa Siku ya Kiyama, nayo ni Siku ya kuwatesa kwa kulipiza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net