Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 77

Az-Zukhruf 43:77

الزخرف

وَنَادَوْا۟ يَـٰمَـٰلِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ ۖ قَالَ إِنَّكُم مَّـٰكِثُونَ

Maana

Nao watapiga kelele waseme: 'Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi!' Naye aseme: 'Hakika nyinyi mtakaa humo humo!'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nao watapiga kelele waseme: Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi! Naye aseme: Hakika nyinyi mtakaa humo humo! [77]

[77] Na wakosefu, watapo kwisha kata tamaa ya kupunguziwa adhabu kali, watamwita Malik, huyo ni askari wa Motoni wakimwambia: Mwombe Mola wako Mlezi atufishe tupumzike na adhabu ya Jahannamu. Na Malik awambie: Nyinyi mtakaa humu humu katika adhabu milele!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hao wahalifu waliomkanusha Allah Mtukufu, baada ya Allah Mtukufu kuwatia kwenye moto wa jahanamu, watamwita Mālik, mshika hazina za Moto, kwa kusema, Ewe Mālik! Basi na Atufishe Mola wako, tupate kupumzika na haya tuliyonayo,” Hapo Mālik awajibu, «Nyinyi ni wenye kukaa, hamna kutoka Motoni na hamna makimbilio ya kujiepusha nao».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net