Az-Zukhruf 43:76
الزخرفوَمَا ظَلَمْنَـٰهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا۟ هُمُ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Wala Sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio waliokuwa madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala Sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio walio kuwa madhaalimu. [76]
[76] Wala Sisi hatukuwadhulumu wakosefu hawa kwa adhabu hii, lakini wao wenyewe ndio walio jidhulumu nafsi zao kwa kukhiari upotofu kuliko uwongofu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hatukuwadhulumu wahalifu hawa kwa kuwaadhibu, isipokuwa wao wenyewe ndio waliojidhulumu nafsi zao, kwa kushirikisha kwao na kukataa kuwa Allah Mtukufu Ndiye Mola wa haki, Aliye Peke Yake, Asiye na Mshirika na kuacha kuwafuata Mitume wa Mola wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net