Az-Zukhruf 43:61
الزخرفوَإِنَّهُۥ لَعِلْمٌ لِّلسَّاعَةِ فَلَا تَمْتَرُنَّ بِهَا وَٱتَّبِعُونِ ۚ هَـٰذَا صِرَٰطٌ مُّسْتَقِيمٌ
Na kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndiyo Njia Iliyonyooka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka. [61]
[61] Na hakika Isa kwa kuzuka kwake bila ya baba, na kuponyesha kwake vipofu na wakoma ni dalili ya kukaribia Saa ya Kiyama. Basi usiwe na shaka nayo. Na fuateni uwongofu wangu na Mtume wangu. Hii ninayo kuitieni ndiyo Njia Iliyo Nyooka yenye kufikilia Uwokovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika kuteremka kwa ‘Ǐsâ, amani imshukie, kabla ya Siku ya Kiyama, ni dalili ya kukaribia kiama, basi msitie shaka kuwa hilo la kiama ni lenye kutokea. Na nifuateni mimi katika yale ninayowatolea habari kutoka kwa Allah Mtukufu Aliyetukuka. Hii ni njia imara inayoelekea Peponi, isiyo na kona kona.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net