Az-Zukhruf 43:60
الزخرفوَلَوْ نَشَآءُ لَجَعَلْنَا مِنكُم مَّلَـٰٓئِكَةً فِى ٱلْأَرْضِ يَخْلُفُونَ
Na tungelipenda, tungeliwafanyia miongoni mwenu Malaika katika ardhi wakifuatana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tungeli penda tungeli wafanyia miongoni mwenu Malaika katika ardhi wakifuatana. [60]
[60] Na lau tungeli taka, tungeli wageuza baadhi yenu, enyi watu, mkawa ni Malaika mkifuatana katika ardhi, kama wanavyo kufuateni watoto wenu, mjue kwamba Malaika wananyenyekea kufuata kudra ya Mwenyezi Mungu. Basi vipi wao wastahiki Ungu?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau tungetaka tungewaleta badala yenu Malaika, hawa baada ya wengine.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net