Az-Zukhruf 43:58
الزخرفوَقَالُوٓا۟ ءَأَـٰلِهَتُنَا خَيْرٌ أَمْ هُوَ ۚ مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًۢا ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ
Wakasema: 'Miungu yetu kwani si bora kuliko huyu?' Hawakukupigia mfano huo ila kwa ubishi tu. Bali hao ni watu wagomvi!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Miungu yetu kwani si bora kuliko huyu? Hawakukupigia mfano huo ila kwa ubishi tu. Bali hao ni watu wagomvi! [58]
[58] Makafiri wamesema: Je! Miungu yetu na Isa, nani bora? Ikiwa yeye yuko Motoni basi sisi na miungu yetu tutakuwa pamoja naye. Hawakupigii mfano huu wewe ila kutafuta ubishi tu, na kushindana kwa maneno, si kwa ajili ya kuitafuta kweli ilivyo. Bali hawa ni watu ambao ni shadidi wa khasama, wamebobea kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na walisema washirikina wa watu wako, ewe Mtume, “Je waungu wetu tunaowaabudu ni bora au ni ‘Ǐsâ ambaye watu wake wanamuabudu? Akiwa ‘Ǐsâ atakuwa Motoni, basi nasi natuwe na waungu wetu pamoja na yeye. Hawakukupigia mfano huu isipokuwa kwa kupinga, bali wao ni wabishi kwa njia ya ubatilifu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net