Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 57

Az-Zukhruf 43:57

الزخرف

وَلَمَّا ضُرِبَ ٱبْنُ مَرْيَمَ مَثَلًا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ

Maana

Na alipopigiwa mfano Mwana wa Mariamu, watu wako waliupigia ukelele.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na alipo pigiwa mfano Mwana wa Mariamu, watu wako waliupiga ukelele. [57]

[57] Na alipo pigiwa mfano Isa bin Maryam katika kuwa kwake kama Adam kwa kuwa Mwenyezi Mungu alimuumba kwa udongo, kisha akamwambia: Kuwa, na akawa, subhanallah. Basi yeye ni mtumwa aliye umbwa, aliye neemeshwa kwa kupewa Unabii, subhanallah. Haifai kumuabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na watu wako wanapuuza hizo sifa zinazo pigiwa mfano, na wala hawafahamu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na washirikina walipopiga mfano wa ‘Ǐsâ mwana wa Maryam walipombishia Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na kumpa hoja kuwa manaswara wanamuabudu, wakawa watu wako wanainua sauti zao na kupiga kelele kwa furaha. Napo ni pale neno la Allah Mtukufu Aliyetukuka lilipoteremka lisemalo: (Nyinyi na vile mnavyoviabudu badala ya Allah Mtukufu ni kuni za Moto, nyinyi nyote ndani ya Moto huo mtaingia.). Na washirikina wakasema, «Tumeridhika kwa waungu wetu wawe na cheo cha ‘Ǐsâ», Allah Mtukufu Akateremsha neno lake lisemalo «Hakika wale ambao ilitangulia kutoka kwetu kuwa wao ni wema, hao ni wenye kuepushwa nao huo Moto». Yule anayetupwa Motoni, miongoni mwa waungu wa makafiri, ni yule aliyeridhika kuabudiwa na wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net