Az-Zukhruf 43:5
الزخرفأَفَنَضْرِبُ عَنكُمُ ٱلذِّكْرَ صَفْحًا أَن كُنتُمْ قَوْمًا مُّسْرِفِينَ
Je, tuache kuwakumbusha kabisa kwa kuwa nyinyi ni watu mliopita mipaka kwa ukafiri?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Tuache kukukumbusheni kabisa kwa kuwa nyinyi ni watu mlio pita mipaka kwa ukafiri? [5]
[5] Je! Tukupeni muhula, tuache kukuteremshieni Qur'ani kwa kukutupilieni mbali, kwa sababu ya kupita kwenu mipaka ya ukafiri juu ya nafsi zenu? Hayawi hayo, kwa kufuata hukumu ya kulazimikana kwenu na hoja.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je tuwape nyinyi mgongo na tuache kuwateremshia Qur’ani kwa ajili ya kupuuza kwenu, kutofuata na kupita mipaka kwenu katika kukataa kuiamini?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net